"Mungu akuweke kwaajili yangu" Hamisa Mobetto amsherehekea mama yake

Hamisa alimtaja mama yake kama mama bora na kumtakia maisha marefu.

Muhtasari

•Wasanii mashuhuri wakiwemo Jacqueline Wolper, Mwijaku, Fayvanny na Kassim Mganga walijumuika na Hamisa kumsherehekea mamake.

•Hamisa vilevile alimsherehekea mama yake kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram na kumtambua kama malkia wake.

Hamisa Mobetto na mama yake
Image: INSTAGRAM// HAMISA MOBETTO

 Mamake mwanamitindo wa Tanzania Hamisa Mobetto, Bi  Shufaa Lutigunga aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa Jumatatu, Desemba 12.

Huku akisherehekea siku hiyo maalum katika maisha yake kupitia mtandao wa Instagram, Bi Shufaa alimshukuru Mola kwa hatua hiyo na kujitakia heri ya siku yake ya kuzaliwa.

"Bi mzuri kazaliwa leo🙏❤," alisema.

Makumi ya wanamitandao walimiminika kwenye ukurasa wa Instagram wa mamake Mobetto na kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa. 

Wasanii mashuhuri wakiwemo Jacqueline Wolper, Mwijaku, Fayvanny na Kassim Mganga walijumuika na Hamisa kumsherehekea mamake.

@mobettohtothetop Happy Birthday mamangu kipenzi.

@wolperstylish Ishii sana mpenzi wangu

@mwijaku Nakupenda.. Nakupenda mama na heri ya siku ya kuzaliwa Mama Mobetto.

Hamisa vilevile alimsherehekea mama yake kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram na kumtambua kama malkia wake.

Huku akimsherehekea, mama huyo wa watoto wawili alimhakikishia mzazi huyo wake kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

"Siku ya Kuzaliwa yenye furaha zaidi kwa Malkia wangu @mama_mobetto nakupenda kutoka kwa mwezi na kurudi" Hamisa alimwandikia mamake.

Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz alimtaja mama yake kama mama bora na kumtakia maisha marefu.

"Mungu akuweke kwa ajili yangu mama yangu .❤️ Nakupenda.  Asante kwa kuwa mama yangu katika kipindi hiki cha maisha na  nikipata nafasi ya kukuchagua katika maisha yangu mengine bado nitakuchagua Mi amor," alisema.

Hamisa alisherehekea siku ya kuzaliwa ya mama yake siku chache tu baada ya yeye mwenyewe kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa mnamo Desemba 10, Hamisa alisema anajivunia mafanikio yake yote maishani.

"Nimewahi kutaka kuwa na zaidi . Ninajivunia na nina furaha kwa kila kitu ulichofanikiwa kufikia sasa. Endelea kuwa na nguvu na usipoteze imani yako kwa MUNGU🙏🏽," Hamisa alijisherehekea kupitia Instagram.

Mama yake pia alimsherehekea kwa ujumbe mtamu na kumhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

"Mama ake na mama kazaliwa leo.. Eee Mungu nasema Ahsante kwa zawadi hiii 🙏🙏❤❤❤❤❤❤," Bi Shufaa alimwandikia bintiye.

"Happy birthday mama ake na mama Nakupenda sana nakuombea maisha marefu mwanangu nakupenda ❤️,