"Tumepoteza ujauzito, nini kilitokea?" Akothee asikitishwa

"Tumepoteza ujauzito 😭😭😭 Maskini Salome Wangu, Nini kilitokea?" alilalamika.

Muhtasari

β€’Akothee alitangaza habari hizo za kusikitisha siku ya Jumamosi na kueleza kuvunjwa moyo kwake na kile kilichojiri.

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwimbaji maarufu Akothee ni mwanamke mwenye huzuni sana baada ya mbwa wake kipenzi Salome kupoteza ujauzito wake.

Akothee alitangaza habari hizo za kusikitisha siku ya Jumamosi na kueleza kuvunjwa moyo kwake na kile kilichojiri.

"Tumepoteza ujauzito 😭😭😭 Maskini Salome Wangu, Nini kilitokea?" alilalamika kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha inayomuonyesha akitumia muda mzuri na mbwa huyo mweupe na  mabaka madogo meusi.

Hapo awali, msanii huyo mwenye umri wa miaka 42  alifichua kwamba Salome ni mjamzito na angejifungua hivi karibuni.

"Salome wetu ni mjamzito sana. Baby Shower ya Salome  niJumapili, nani anakuja na mbwa wake?" Akothee  alisema mnamo Septemba 28.

Machapisho mengi ambayo mama huyo wa watoto watano amefanya kuhusu mbwa wake yanaonyesha uhusiano wao wa karibu. Salome anaonekana kuwa kipenzi chake kati ya wanyama wote aliowafuga.

Mapema mwaka huu, Akothee pia alikuwa ameashiria nia yake ya kupata watoto zaidi na hata kudokeza kuhusu kufanyiwa utaratibu wa kurutubisha mayai yake. Kufikia sasa ana mabinti watatu na wavulana wawili.

Mwezi Julai mwaka huu, mwimbaji huyo alitembelea hospitali moja nchini Ufaransa ambapo alisema alikuwa ameenda kwa ajili ya upanzi wa mbegu ya kiume kwenye tumbo yake ya uzazi. Kuthibitisha madai yake , Akothee alichapisha picha akiwa  hospitalini tayari kwa shughuli hiyo kufanyika.

Wakati huo, aliweka wazi kuwa mtoto atakayemzaa atakuwa na baba lakini atamficha kutoka kwa wanamitandao.

"Tupo kwa daktari leo. Na  mtoto wetu ana baba. Ni kwamba hautawahi kumuona kwenye mitandao ya kijamii, hapa kuna uchawi wa mahusiano," Akothee alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 42 pia alidokeza kuwa angependa kupata mapacha kwa kuwa ana hamu ya watoto.