"Unakaa vizuri sana" Huddah Monroe asifia sura ya Mulamwah baada ya kukutana naye

"@huddahthebosschick unakaa mzuri zaidi ana kwa ana ❤ ," Mulamwah alimjibu.

Muhtasari

•Huddah alisifia mwonekano wa mchekeshaji huyo baada ya kukutana naye ana kwa ana siku chache zilizopita.

•Wasanii hao wawili walikutana katika moja ya hafla ya hivi majuzi.

Image: INSTAGRAM// HUDDAH MONROE, MULAMWAH

Mwanasoshalaiti na mfanyibiashara wa Kenya Huddah Monroe amembwagia sifa kemkem mchekeshaji David Oyando almaarufu  Mulamwah.

Huddah alisifia mwonekano wa mchekeshaji huyo baada ya kukutana naye ana kwa ana siku chache zilizopita.

"Unakaa vizuri sana, ilikuwa vizuri kukutana nawe," alimwambia Mulamwah kwenye mtandao wa Instagram.

Mwanasoshalaiti huyo alikuwa akitoa maoni chini ya chapisho moja la matangazo la Mulamwah kwenye Instagram.

"Leo naskia fiti," Mulamwah aliandika chini ya picha yake akikula pipi.

Mchekeshaji huyo ambaye alionekana kufurahishwa sana na ujumbe wa Huddah pia alisifia urembo wa mwanasoshalaiti huyo.

"@huddahthebosschick unakaa mzuri zaidi ana kwa ana ❤ ," alimjibu.

Wasanii hao wawili walikutana katika moja ya hafla ya hivi majuzi, siku chache baada ya Huddah kuvunja ukimya wa muda mrefu.

Huddah alijitokeza tena baada ya ukimya wa miezi miwili mapema mwezi huu. Mwanasoshalaiti huyo hakuwa ameonekana kwenye mitandao ya kijamii kwa takriban miezi miwili, jambo lisilo kawaida yake.

Huu ndio muda mrefu zaidi ambao amewahi kutoweka kwenye mitandao ya kijamii kwani tangu kujizolea umaarufu mkubwa miaka kadhaa iliyopita amekuwa akitumia kurasa zake kufanya matangazo ya kibiashara na kama jukwaa la kuzungumza kuhusu masuala mbalimbali ya kimaisha.

Wakati akirejea, kipusa huyo alizindua rasmi duka lake la vipodozi la Rich Beauty. Hili ni duka la kwanza kabisa ambalo sosholaiti amefungua.

"Asante nyote kwa kunijulia hali. Nimekuwa nikishughulika kutatua maisha yangu," alisema katika chapisho la kwanza baada ya kurejea.

Haya yanajiri huku Mulamwah akidaiwa kuwa kwenye mahusiano mapya na msanii wake Ruth K. Tetesi za mahusiano yao zilifufuliwa upya baada yao kuhudhuria hafla pamoja huku wakiwa wameshikana mikono.

"Juzi bestie alinipeleka out, halafu kila mtu akaenda kwake. Asante sana bestie @atruthk. Sikuwa nimewahi kula saviet," Mulamwah alisema kuhusu date yake na Ruth.

Mulamwah alitangaza kutengana na mzazi mwenzake Carrol Sonnie mwaka jana, siku chache tu baada yao kumkaribisha binti yao duniani.