Chama cha ODM chamwonya Musalia Mudavadi dhidi ya kujipendekeza

Nasa Principals
Nasa Principals
Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna amemshambulia kwa maneno kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi kutokana na matamshi yake ya awali kwa kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga.

Musalia Mudavadi alitamka kwamba Raila Odinga ni "Kizingiti kikuu katika siasa ya Kenya"

Edwin Sifuna alimwonya naibu waziri mkuu huyo wa zamani kukoma kumshambulia kiongozi huyo.

Kutokana na ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, chama cha ODM kilimwonya Mudavadi dhidi ya kutoa  matamshi yasiyofaa kwa kiongozi wa chama hicho.

https://twitter.com/TheODMparty/status/1191740325800415233?s=20

Aidha, waziri huyo wa zamani wa Fedha alimshtumu Raila kwa kuwalinda viongizi fisadi.

Alisema kwamba baadhi yao tayari wanachunguzwa na idara ya DCI pamoja na tume ya EACC.

Musalia alinuia kumaanisha gavana wa Makueni Kivutha Kibwana, gavana wa Kitui Charity Ngilu na Anne Waiguru wa Kirinyaga ambao walimpgia kampeni mgombea wa chama cha ODM Imran Okoth.

Hata ingawa hakuna kati yao aliyeshtakiwa, wote wamewaihojiwa na tume ya EACC.

"Niliwaona magavana wengi hapa. Wengi wao wamefuja fedha za serikali za kaunti na faili zao zimo katika afisi za DCI na EACC. Wao wanajaribu kupata ulinzi kutoka Raila dhidi ya uchunguzi dhidi ya uchunguzi unaondelea," Mudavadi alisema alisema.

Mudavadi alilalamika kwamba Raila hakuwa na shukran kutokana na mchango wa chama cha ANC kwao kwa miaka mingi na sasa anasaka usadizi kwingine huku akiwaacha.

"Muda wake umeisha, taifa lote linajua kwamba Raila amekuwa akiwatumia wengine miaka ya 2013 na 2017. Kwa sasa anajaribu kufanya hivy Kibra," Mudavadi alisema.

Uchaguzi wa Kibra umevutia wagombea 24, huku vyama vya ANC, Jubilee na ODM vikipigani kuonesha ubabe katika eneo hilo.

Hata hivyo, chama cha ODM kinapigani kudumisha kiti hicho kilichoachwa wazi baada ya kifo cha Ken Okoth kilichotokea Julai.