Chifu akabiliwa na mashtaka ya kuiba mbwa wa askofu Nyeri

unnamed (1)
unnamed (1)
Chifu Paul Gachiri Wageni, 55, alifikishwa mbele ya mahamaka ya Othaya jana kwa shutuma za wizi wa mbwa wawili wa mhubiri Thomas Wahome wa kanisa la Helicopter hapa jijini Nairobi.

Chifu huyu wa kata ndogo ya Kiandemi anaaminika kuwa aliwaiba mbwa hawa wakiwa katika ulinzi wa Stephen Macharia Ndichu katika boma la mhubiri huyu.

Soma mengine hapa:

Baadaye mlinzi huyu aliripotia bosi wake kuwa mbwa wawili wa kiume na kike wamepotea. Kwa mujibu wa stakabadhi za upande wa mashtaka, Askofu Thomas aliwanunua mbwa hao kutoka nchi jirani ya Tanzania mjini Arusha mwezi wa Disemba 2014, kwa bei ya elfu mia tatu kila mbwa.

Mahakama ilimwachilia Gachiri kwa dhamana ya fedha 200  huku kesi yake ikiratibiwa kusikilizwa juni tarehe nne mwakani.

Soma mengine hapa:

Chifu huyu alijitetea kwa afisa wa upelelezi Willy Bisnei kuwa aliwanunua mbwa hawa kutoka kwa mama wahome, Antonia Njambi mwezi wa machi 2013 kwa shilingi 200 kila mmoja.