Chuo kikuu cha Nairobi chapata Naibu Chansela mpya

mbeche.2.jfif
mbeche.2.jfif
Profesa Isaac Mbeche Meroka ameteuliwa kaimu Naibu Chansela wa chuo kikuu cha Nairobi. Kuteuliwa kwa Mbeche kunafuatia kukamilika kwa muda wa kuhudumu wa Profesa Peter Mbithi.

Kabla ya kuteuliwa kwake Mbeche alikuwa Makamu wa Naibu wa Chansela akisimamia maswala ya elimu na maslahi ya wanafunzi.

Mbithi anatarajiwa kwenda kwa likizo ya kustaafu kabla ya muhula wake kukamilika mwezi Januari mwakani wakati naibu chansela mwingine atateuliwa.

Mbeche alizaliwa mwaka 1952 na ana shahada ya elimu kutoka chuo kikuu cha Nairobi, shahada ya uzamili kutoka chuo hicho na Shahada ya uzamivu (PHD) katika sayansi ya usimamizi kutoka chuo kikuu cha Lancaster nchini Uingereza.