Conjestina ana machungu sana kuhusu kutengwa na kutopokea usaidizi wowote na serikali-Carol Radull

Carol Radull  hivi maajuzi alimtembelea mwanabobdia wa zamani wa Kenya Conjestina  chien’. Ziara hiyo imefungua hisia nyingi kali huku wengi wakishuhudia jinsi usaliti unavyoweza kumpata gwiji yeyote amabaye anajituma kuiwakilisha nchi hii katika ulingo wowowte hasa katika sanaa na spoti .

Conjenstina  alikuwa nyota wa Kenya na  miaka ya 2000 aliwasha nyota ya Kenya katika ulingo wa ndondi kwa upande wa akina dada lakini  hali yake  imekuwa ikidorora bila hatua yoyote kuchukuliwa na maamlaka husika kuanzia kwa serikali hadi kwa wasimamizi wa michezo .

Mambo hayakuwa mazuri kwa staa huyo  wa zamani wa ndondi na mara ya mwisho wakenya wengi walisikia kumhusu ni wakati  gavana wa Nairobi Mike Sonko  alipomtoa Siaya na kumpleka kwa matibabu  mwaka wa 2019.

Radull  alipiga picha kadha na Conje ambazo zinaonyesha taswira ya kuvunja moyo   na alieleza jinsi Conje mwanzoni alivyokuwa na hasira walipokutana lakini akatulia baada ya wao kuzungumza kwa muda . Pia amesem kwamba mwanandondi huyo amepoteza uzani  huku  akionyesha kwamba bado anapenda sana medali alizoishindia kenya kwani amezihifadhi kwa njia nzuri .

Carol  alisema kwamba Conje alihisi kuachwa na maamlaka husika za michezo katika wakati wake mgumu ambapo msaada kwake ungekuwa jambo la muhimu sana ili kuyabadilisha maisha yke .

Baada ya  ujumbe huo wa Radull  watu wengi na wahisani wamejitokeza wakitaka kumsaidia Conje lakini wasichofahamu watu ni kwamba Conje anahitaji makakati wa muda mrefu unaoweza kuhakikisha kwamba harejei  tena katika mazingira mabyo yanamtia katika hatari ya kujitumbukiza katika utumizi wa dawa za kulevya na msongo wa mawazo bali anahitaji njia ya kuweza kuitumia talanta yake na kuhisi kuhudumia tena nchi yake .