Corona,Takwimu za sasa kuhusiana na Corona Ulimwenguni

NA NICKSON TOSI

Kulingana na shirika la afya Duniani WHO,mataifa takriban 196 yameathirika pakubwa kutokana na virusi vya Corona huku makampuni na biashara zikiendelea kusajili hasara kila siku.

Kufikia sasa WHO imeripoti kuwa watu takriban 1000,000 ulimwenguni wameambukizwa virusi hivyo huku watu 51000 wakisemekana wamepoteza maisha yao hadi sasa.

Kwa sasa taifa la Amerika linaongoza kwa maambukizi ya kila siku huku likiwa limesajili visa vipya vya maambukizi kuwa 216,500 na watu takriban 5,100 wakiwa wameaga dunia.

Taifa la Ufaransa chini ya masaa 24 limesajili vifo vya watu 471 na Uingerza nayo ikiendelea kurekodi idadi kubwa ya vifo ikiwa 2,921 ikiashiria asilimia 24 ya vifo kwa taifa hilo kufikia sasa.

Bara la Afrika kufikia sasa limesajili visa 6,860  na vifo 269 ,taifa la Afrika Kusini likiwa linaongoza kwa maambukizi.

Jedwali lifuatalo limeelezea idadi kamili ya visa vya Corona bara la Afrika ,japo visa hivyo vinabadilika kadri mataifa yanavyoendelea kusajili idadi mpya kila siku.

Kenya kwa sasa imeandikisha visa 110 vya watu kuambukizwa na Corona ,watu 3 wakiwa wameaga dunia na watu 4 wakiwa wamepona ama kupata nafuu na kuruhusiwa kwenda nyumbani.