Covid-19: Kenya yasajili visa ,278, vipya vya maambukizi ya corona

mercy mwangangi
mercy mwangangi
Kenya hii leo imesajili visa 278 vipya vya maambukizi ya virusi vya corona,na kufikisha idadi ya watu 9726 walioathirika na virusi hivyo hii ni kutokana na sampuli 1403 vilivyofanywa chini ya masaa ishirini na nne na kufikisha idadi ya sampuli 207,987 zilizopimwa nchini.

Katibu msimamizi katika wizara ya afya Mercy Mwangangi amesema ia hii leo wagonjwa 99, wameruhusiwa kuenda nyumbani na kufikisha 2832 waliopona kutokana na virusi hivyo.

Akizungumza akiwa katika kaunti ya kwale Mercy amempongeza gavana wa kwale kwa kazi nzuri ambayo ametenda ili kpigana na virusi vya corona huku akiwashukuru maafisa wa afya kwa kazi yao.

Kufikia sasa kaunti hiyo imesajili visa 139 vya maambukizi kutokana na sampuli 1598, na kusema kuwa wote walioambukizwa wamepona isipokuwa wagonjwa tisa ambao wanazidi kupokea matibabu wakiwa manyumbani mwao.

Wagonjwa,3, hii leo wamepoteza maisha yao kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 184 Mercy Mwangangi alisema.

Kaunti ya Nairobi inazidi kuonoza katika maambukizi ya virusi hivyo