Irene Nduta mwenye umri wa miaka 50 ni mama mwenye huzuni na amelia hadi amekauka macho tangu binti yake Anne Wachuka mwenye umri wa miaka 25 alipowasili nchini Kutoka Dubai siku ya Jumatatu na kutua katika uwanja wa JKIA .
“ Nilikuwa nimeenda kumpokea lakini nilipomuangalia, hakuwa sawa. Alionekana kuwa na mawazo’ Nduta amesema .
Nduta anasema kabla ya binti yake kuja Kenya akiwa Dubai, alifahamu kwamba hali yake kiakili haikuwa nzuri kwani alipigiwa simu kuambiwa kuhusu hali yake. Wafanyikazi wenzake walikuwa wamesema kwamba Wachuka alikuwa mgonjwa na alikuwa amelazwa hospitalini.Walimueleza kuwa binti yake hakuwa na nguo na hakuna aliyekuwa akimtunza . Akikumbuka taswira hiyo ya mtoto wake, Nduta anabubujikwa machozi kwani kando na hali ya mwanawe, pia ana ufahamu kwamba Wachuka na wakenya wengine waliokuwa wakifanya kazi ya usafi huko Dubai walikuwa wakiteswa na mwajiri wao .
Nduta alimpigia wakala aliyempeleka binti yake Dubai ili kujua kinachofanyika lakini akapuuza akisema binti yake alikuwa tu akifanya maigizo kwa sababu aliharibu vitu vya kampuni aliokuwa akiifanyia kazi . Baadaye Nduta alipokea simu ya daktari mmoja kutoka Dubai aliyemuambia kwamba binti yake alikuwa mgonjwa na anahitaji msaada wa familia yake .
“ Daktari alipompa mtoto wangu simu Anne alisema tu ‘nakuja mama, nakuja mama’… mananeno hayo yalinivunja moyo’ anasema. Nduta akibubujikwa machozi. Baadaye Nduta aligundua kwamba alihitaji sasa kumtumia Wachuka nauli ya kurejea Kenya .
Nduta anasema walipofika uwanja wa ndege wa JKIA , watu wote waliokuwa wakiwasili nchini walikuwa wakipelekwa katika taasisi za serikali kwa uangalizi kwa siku 14 kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani. Anne alipelekwa katika chuo cha KMTC Nakuru . “ Katik chuo cha KMTC niliwarai polisi waniruhusu nimtunze lakini walikataa. Wasamaria wema walinipia simu wakiniambia kwamb Anne likuwa akilala nje ya jengo katika Corridor’ amesema. “ Mbona serikali inamazui aondoke ili tumpe utunzi? Je, nitaweza kungoja kwa siku 14 kabla ya kumuona mtoto wangu? Serikali inafaa kunisaidia tafadhali ‘ anasema Nduta .
Nduta ambaye sasa amelazimika kuishi Nakuru na jamaa yake akingoja kuachiliwa kwa binti yake anasema amekuwa akiwatuma binti yake mwingine na kakake yao kwenda kumuona Anne lakini hawaruhusiwi kuingia ndani .
" Siwezi kumtembelea kwa sababu ya umri wangu. Binti yake ameogopa kwa sababu iwapo walio ndani wana virusi vya Corona basi nitaangamia’ anasema Nduta .