Covid-19 sio kikwazo kwa kura ya maoni –viongozi wa Magharibi

western leaders
western leaders
Wakenya wanafaa kujitayarisha kwa kura ya maoni licha ya kuwepo janga la corona  viongozi kadhaa kutoka magharibi wamesema .wakiongozwa na aliyekuwa maneja wa kampeini za gavana Wilber Otichilo Joseph Simkha  ,viongozi hao wamesema wakenya wanafaa kuzoea maisha  licha ya kuwepo kwa virusi hivyo  na nidhamu ya hali ya juu itahitajika ili kuzuia maambukizi zaidi .

Wanatataaluma hao walikuwa wakizungumza Ebunangwe Resort  katika eneo bunge la siku ya ijumaa .

" Mataifa mengine yameandaa uchaguzi wakati huu  wa corona .Ufaransa  na Malawi zimefanya hivyo vizuri na Tanzania pia huenda inaelekea kuchukua hatua kama hiyo’ amesema Simekha .

“ iwapo wakenya watapewa fursa ya kupiga kura ,wasipuuze maagizo ya serikali kuhusu coronavirus ,tumeona athari za virusi hivyo kote duniani’ alisema

Kuhusu mchakao wa BBI Simekha  amesema sio tu kuhusu uongozi bali pia ni njia yay a kuboresha uchumi wa taifa .

Wanataaluma  hao wamesema kuna haja ya kuwahusisha katika mchakato huo mzima  ili kuzuia wanasiasa kuwapotosha waenya . wameongeza kwamba BBI inalenga kuimarisha ugatuzi .