Covid-19: Watu,12 wafariki huku,544, wakipatikana na virusi vya corona

Watu,544, hii leo wamepatikana na virusi vya corona katika saa 24 zilizopita huku idadi ya walioambukizwa nchini ikiongezeka na kufikisha jumla ya 19,125 walioambukizwa virusii hivyo.

Huku hayo yakijiri watu 12 wamepoteza maish yao kutokana na virusi hivyo huku idadi ya jumla ya 311 ya watu walioga dunia, katika visa hvyo vipya 340 ni wanaume huku 204 wakiwa wanawake.

Watu 113 wameruhusiwa kuenda nyumbani waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema.

Waziri wa afya Mutahi Kagwa alsiema huenda kuongezeka kwa wanaopatwa na maambukizi ni kutokana na msimu huu wa baridi. Aidha Mutahi alionya kuwa idadi ya maambukizi kwa wanawake imeanza kupanda ikilinganishwa na hapo awali.

"Tunaona idadi ya kina dada ambao wanaambukizwa imeanza kuongezeka. Hatujui ni tabia zimeanza kubadilika ua ni nini," alisema Kagwa