Covid-19: Watu,83 wapatikana na corona huku 72 wakipona

Hii leo kenya imesajili visa 83 vipya vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi jumla ya 35,103 kutokana na sampuli 3,093 zilizopimwa kwa saa 24 zilizopita.

Katika maambukizi hayo mapya 77 ni wakenya huku 6 wakiwa raia wa kigeni,58 ni wanaume ilhali 25 ni wanawake amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe.

Nairobi inazidi kuongoza katika maambukizi hayo huku leo ikisajili visa 27 hukuikifuatwa na kaunti ya busia na visa 15.

Vile vile watu 72 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 21,230 ya watu waliopona kutokana na virusi hivyo,39 wamepona wakipoea matbabu ya nyumbani na wengine 33 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti huumu nchini.

Pia watu 3 wamepoteza maisha yao kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 597 ya watu walioa dunia kutokana na virusi vya corona.