COVID 19:Kenya yasajili visa 104 vya coronavirus na kufikisha jumla ya visa 4,478

Visa vipya 104 vya coronavirus vimeripotiwa nchini katika saa 24 zilizopita baada ya sampuli  2,820  kupimwa.

Katibu wa utawala wa wizara ya Afya  Rashid Aman  amesema kwa jumla Kenya imefanya vipimo vya sampuli  136,361  hadi kufikia sasa

Kati ya visa hivyo vipya 76 ni vya wanaume ilhali 28 ni vya wanaume huku aliye na umri wa juu zaidi akiwa na miaka 76 .

Nairobi  inazidi kuongoza kwa idadi ya juu ya visa hivyo  baada ya 60 zaidi kuripotiwa kati ya 104 vya hivi leo  Mombasa   ina  33, Kilifi 5, Busia 3, Kajiado 2  na  Taita Taveta  1.

Mjini ,  visa hivyo ni kama ifuatavyo katika mitaa  : Langata 22, Kibra 19, Westland 11, Starehe 3, Dagoretti North 2, Embakasi South, Embakasi East  na  Kasarani  kisa kimoja kila mtaa .

Idadi ya walioaga dunia kwa ajili ya virusi hivyo sasa ni  watu 121  baada y watu 2 zaidi kuaga dunia . watu 36 wamepona ugonjwa huo na kufikisha jumla ya walipona kuwa  1586 .