Daah! DJ Nyc afunguka jinsi wanaume wanamuona kama tishio

dj nyc
dj nyc
Ama kwa hakika, kazi ni kazi na hata kama kazi za uDJ hujulikana kuwa za wanaume, siku hizi mabinti pia, wamebobea sana na hata kuonekana kama tishio kwa djs wa kiume.
Dj mufti sana wa Radio Jambo, Dj Eunice Wanjiku ambaye hujulikana sana kama Dj Nyc, ni baadhi ya ma dj ambao wanawapa kiwewe ma dj wa kiume kwani binti huyu anaielewa kazi yake vilivyo.
Nyc alisema kuwa, tangu utotoni, ndoto yake ilikuwa kufanya kazi kwenye radio na akaona njia rahisi zaidi ya kufanya kazi kwa radio ni kuwa Dj.
Hata hivyo, Dj Nyc alisomea kozi ya afya ya jamii, (public health) alipokuwa kwenye chuo kikuu, lakini hakuwa anaipenda kozi ile.

Katika mahojiano na Word Is, Dj Nyc alisema kuwa alipojiunga na chuo kikuu, alifanya kozi ya afya ya jamii (public health) lakini baada ya kufanya 'assigment 'moja, iliyokuwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti, alielewa fika kuwa, haapendi kazi ile, na anataka kuwa Dj.

“I went to do public health and the first assignment was in a morgue, which was not my thing. That pressure made me like the DJ part more.” Dj Nyc alisema.

Baada ya hayo ,Nyc alimpigia baba yake simu na kumwambia kuwa anataka kufanya kazi kwa radio na njia ambayo itamwezesha afanye kazi kwa radio ni kama atakuwa Dj.

Kwa mara ya kwanza, baba yake alikataa ombi lake lakini baada ya kusisitiza kuwa ile kazi ndio kazi ambayo anataka, baba yake alimlipia karo ya shule ya kusomea kuwa DJ baada ya kumhakikishia kuwa, atamaliza kozi yake ya afya ya jamii.

“At first he stopped me but I convinced him, and he paid my fees after I promised to finish my public health course,” Nyc alisema.

Nyc alikazana na kusoma kozi yake ya afya ya jamii na pia udj na baada ya miaka minne, alihitimu na kozi hiyo ya afya ya jamii. Hata hivyo, alisema na kusisitiza kuwa, hajawahi tumia digrii ile na mpaka wakati  huu, mama yake humwona kama binti asiye na kazi.

“I have never used the degree anywhere and my mum still thinks I’m jobless.”

Safari ya udj, haijakuwa rahisi, kwani dj wengi wa kiume huwaona dj wa kike kuwa tishio kwao na kwa hivyo, wanakutishia na wengine kutaka kushirikiana na wewe kimapenzi ili wakupe kazi.

 “There is discrimination in the industry as some male DJs see you as a threat and try to fight you while others want to [sleep with you] to give you gigs,” alisema.
Zaidi ya hayo, Nyc alisema kuwa, ni vigumu sana kupata mpenzi kwani, wanaume wengi huogopa kumchumbia binti anayefanya kazi usiku kwani kazi yao huwabidi waende wafanye kazi usiku.
Vilevile, Nyc alisema kuwa kufanya kazi na Mbusi na Lion ni kitu bora sana kwani watu hawa, wamemsaidia vilvyo .
“They are the best duo to work with and through them, I am now known and they have been helping me get gigs,” Nyc alisema.
Mwisho, ujumbe wake kwa mabinti wanaotaka kuwa Dj ni kuwa wajue kwamba mambo hayatakuwa rahisi wanapoanza kazi hii lakini kuangazia, na kuzingatia yale ambayo unataka kupata maishani ndio ufunguo wa kufaulu kama dj wa kike.

"It won’t be easy at the start, but focusing on what you want to achieve is the key.”Dj Nice alisema.