"Daktari Wanatumia Mulika Mwizi Wakifanya Upasuaji" Dkt Moseti Asimulia (AUDIO)

daktari moseti
daktari moseti
Baada ya mahakama kuagiza madaktari waliofungwa gerezani kwa madai ya kukiuka agizo la mahakama kusitisha mgomo ili kufungu njia ya mazungumzo kati yao na serikali, kuwachiliwa, daktari Moseti alizuru studio zetu na aliyosimulia yaliwaaacha wengi akiwemo mtangazaji, Massawe Japanni vinywa wazi.

Kulingana na daktari Moseti, licha ya wengi kudhni kuwa wanayotaka tu ni nyongeza ya mishahara, kuna mengi ambayo wanapigania ambayo yatakuwa kwa manufaa yao na pia wananchi kwa jumla.

Je uliwahi jua kuwa kuna madaktari ambao wamevamiwa na kuuwawa wakitoka kazini kuokoa maisha ya watu au madaktari ambao wameteseka kwa kiwango cha kutumia mwanga wa simu ya aina ya 'Kabambe' ili kufanyia wagonjwa upasuaji?.

Basi bwana Moseti alisimulia yote ambayo yanavunja moyo.

"Kwa kweli mkataba wa CBA ni kitu ambacho kinafaidi mwananchi wa kawaida kama madawa, vifaa vya hospitali." Alieleza Dkt Moseti.

"Ukiingia katika mitandao ya kijamii utapata habari nyingi za jinsi madaktari wanavyoteseka, kuna picha kadhaa zinaonyesha madaktari bila stima na inabidi wanatumia mulika mwizi ili kufanya upasuaji, madaktari hawana glovu inabidi wanatumia mikono yao na hatujui mgonjwa ana magonjwa gani.."

Pata uhondo kamili katika kanda ifuatayo.

https://soundcloud.com/ken-odero-209313547/dr-moseti-interview-with-radio-jambo-on-cba