DCI hafuata mabenki, safaricom kwa sababu ya shambulizi la Dusit

1883002
1883002
Mkurugenzi wa uchunguzi wa tuhuma George Kinoti azingatia mashtaka dhidi ya maafisa wa idara ya usimamizi ya CBK, kituo cha taarifa za fedha, idara ya usimamizi ya safaricom M-pesa.

Wachunguzi wanaendelea kuchunguza vile millioni 9 zilitumika ili kufanikisha shambulizi la Dusit zilizo tumwa kwa njia ya M-pesa.

Kitengo cha polisi cha kupambana na ugaidi kina rada juu ya benki ya Kenya CBK, kituo cha taarifa za fedha, benki ya Diamond Trust na Safaricom juu ya shambulizi ambalo lilitokea January 15 na kusababisha vifo vya watu 21.

Polisi wa uchunguzi walisema kuwa  mashtaka maalum itaamua kupitia ushahidi na makosa yaliyotokea katika kila taasisi.

"Tutaenda katika kila mtu ambaye ako kwa kila sekta ya benki katika mtandao wa uhamasisho wa pesa wa rununu ambao ilitumika," Kinoti alisema.

Hakusema ni lini kushikwa na mashtaka yatafanyika ilhali uchunguzi ulikamilika na faili kupelekwa kwa mkurugenzi wa mashtaka Noordin Haji kuweza kupeana ruhusa.

"Sidhani tumefanya makosa, watu hutumia M-pesa kuleta pesa nchini na kisha kutoa kupitia utaratibu wa standard,"Aliongea Collymore.

Mkerugenzi mkuu wa Safaricom jana alithibitisha kuwa kikundi cha Safaricom kiliweza kukutana na DCI wiki iliyopita kisha kumueleza utaratibu ambao hutumika katika M-pesa.

"Tuhuma za shughuli zinaripotiwa kwa kituo cha taarifa za fedha, kama tunaona shughuli ambazo hazifai kutoka kwa nchi fulani, tuta faili ripoti za tuhuma za shughuli,

"Tuliweza kufaili ripoti ya STRs katika shughuli za Dusit, pia tuliweza kuachisha M-pesa till zao kabla ya shambulizi la DusitD2," Alisema Bob.

Katika uchunguzi wa awali ulifichua kuwa mmoja wa magaidi Hassan Nur aliweza kupokea millioni 9 kutoka Afrika kusini kupitia M-pesa zaidi ya miezi mitatu, kisha pesa hizo kutumwa Somalia ambapo magaidi hao walikuwa.

Nur alikuwa na agenti za M-pesa 52. Agenti 47 zilisajiliwa katika mwezi wa Oktober na Desemba mwaka jana kila moja ikiwa na laini tofauti huku akiwa amesajili laini hizo na vitambulisho tofauti.

Shughuli hizo ziliweza kufanyika kupitia benki ya DTB maeneo ya Eastleigh, huku meneja wa benki hiyo Sophia Mbogo akijipata mikononi mwa polisi kwa kuto ripoti thuma za shughuli hizo zilizofanyika katika benki hiyo.

Wiki iliyopita maafisa wataasisi hizo waliweza kukutana na DCI ilikujibu maswali kuhusiana na shughuli hizo, swali ni je nani ako na makosa katika mashtaka haya,

Na ukweli utaweza kupatikana?