Dennis Itumbi atetea kitendo cha kufurushwa jukwaani, apondwa Twitter

Mwanablogu na mwanastratejia wa kidijitali katika ikulu hatimaye ameeleza tukio la kufurushwa katika jukwaa wakati ripoti ya BBI ilikuwa ikiwasilishwa kwa wananchi jana Jumatano.

Dennis Itumbi alijipata taabani baada ya kusukumwa kutoka kwenye jukwaa na afisa wa polisi.

Kitendo kimewafanya wengi wazungumze katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Wengi wanahoji kuwa Itumbi ni afisa katika ikulu ya rais na kwa hivyo haikuwa busara kutolewa katika sehemu hiyo.

Aidha, Itumbi amewajibu kupitia mtandao huo,

"Askari alikuwa kazini. Itumbi kazini pia. Sote tulikuwa kazini...Wacha polisi afanye kazi yake... Mimi ni mtu mdogo sana....I have only one advantage, Inshallah, TIME! Haya turudi kwa mambo ya nchi... Salute! Mr. Muriithi, you did well," Alichapisha katika mtandao wa Twitter.

Mwingine na ambaye alijipata katika balaa ni kiongozi wa wengi Murkomen.

Murkomen alinyamazishwa na hadhira baada ya kutilia shaka jinsi maoni kinzani katika ukumbi huo yalilengwa.

"Mimi kama kiongozi lazima niseme, siwezi kusimama hapa nitarajiwe kupigia upato siasa mbaya. Waandalizi wa hafla hii wameipanga kwa njia ambapo watu wenye maoni tofauti wamefungiwa nje," alisema Murkomen.