Dennis Itumbi Kizimbani tena kwa mashtaka mapya ya barua ghushi

Dennis Itumbi
Dennis Itumbi
Mtaalamu wa kidijitali anayehudumu katika afisi ya naibu wa rais Dennis Itumbi na mshahidi Samuel Gateri wameshtakiwa upya kuhusiana na barua ghushi iliyoelezea jaribio la kumuua Naibu wa Rais William Ruto.

Wawili hao walishtakiwa Jumanne baada ya upande wa mashtaka kujumuisha kesi zao kuwa moja. Walikana mashtaka ya kuchapisha taarifa ya uwongo kinyume na sheria.

Mnamo au kabla ya  Juni 20, wanadaiwa kuchapisha barua ya tarehe 30 Mei, 2019 kwa nia ya kusababisha  taharuki kwa umma.

Kulingana na hakimu mkuu mkaazi, Martha Mutuku, masharti ya dhamana ya awali ya pesa bado.

Kesi hiyo itasikilizwa Novemba 18.

Mwezi uliopita, Gateri alishtakiwa na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh 100,000. Gateri alishtakiwa katika korti ya Milimani na kuunda hati bila mamlaka halali.

Gateri alidai kutoa barua Mei tarehe 30 akiwasilisha kwamba alikuwa amesainiwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri katika njama za uwongo za kumuua Naibu wa Rais William Ruto.

Katika kesi tofauti, alishtakiwa kwa kuchapisha taarifa ya uwongo akikusudia kusababisha wasiwasi kwa umma.

Gateri alikana mashtaka hayo mbele ya hakimu mkuu Francis Andayi na akaachiliwa kwa dhamana.