Dereva mjanja! Seneta wa zamani wa Wajir alaghaiwa gari lake hadharani

Ali-e1593162495680
Ali-e1593162495680
Seneta wa zamani wa kaunti ya Wajir Abdirahman Ali Hassan ameandikisha taarifa kwa polisi baada ya dereva wake kuamua kuhepa na gari lake lililokuwa na  milioni 2.1 kando ya kiti.

Hassan, katika taarifa aliyoandikisha kwa polisi, imesema dereva wake Joel Musyoka Jumatano alimfikisha katika eneo la KICC mida 3.30 jioni kwa mkutano.

Alipomaliza mkutano huo na kurejea nje, alishtuka alipopata hakuna Musyoki ambalo lilikuwa na milioni 2.1.

Aidha gari hilo lilipatikana likiwa limeachwa eneo la Nyayo House huku pesa zilizokuwemo zikikosekana.

Maafisa kutoka DCI kwa sasa wameanzisha uchunguzi.