TANASHA7__1___1561360136_69462

Diamond Platinumz ataoa marsharti ya sherehe ya 707

Diamond Platinumz ametoa masharti yatakayo fuatwa ili kuingia kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mamayake pamoja na mpenziwe.

Kwenye mtandao wake wa instagramu, platinumz amesema kuwa watakaohudhuria lazima wawe na mavazi ya rangi Nyeusi, Nyeupe au rangi ya dhahabu.

“Tarehe saba mwezi wa saba ni siku spesheli kwangu kwani mpenzi wangu na mamangu watakuwa wakishereheke siku zao za kuzaliwa. Basi Dress Code ya siku hiyo ni rangi nyeusi, nyeupe na ya dhahabu. Atakaye kuja na rangi nyingine basi hataruhusiwa kuingia.”

Nasib Abdul Juma maarufu kama Diamond Platinumz kwa sasa anatesa kwa kibao chake kinachoitwa Kanyaga. Tarehe saba mwezi wa saba ni siku spesheli sana kwake Diamond Platinumz kwani ndiyo siku ya kuzaliwa kwake Mpenziwe Tanasha na mamaye mzazi Dangote.

diamond

Sherehe hio itafanyika eneo la Mlimani City Jumapili tarehe saba mwezi wa saba.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments