thumb_nqtqrtm6mzcdapqbyh5ac4aad086b3a

Diamond Platnumz afunguka baada ya simu ya rais Pombe Magufuluni stejini

 

Msanii wa mkubwa Afrika Diamond Platnumz amefunguka muda mchache baada ya kupigiwa simu stejini na rais Pombe Magufuli.

Rais wa nchi jirani ya Tanzania John Pombe Magufuli aliwavutia wengi kwa tukio la kumpigia simu staa mkubwa Diamond Platnumz kipindi na ambapo alikuwa akitumbuiza stejini.

Image result for diamond magufuli

Toka Nenda zako! Mastaa waliowahi kufukuzwa vilabuni

Katika tamasha kubwa lililofanyika Kigoma, msanii huyu alikuwa anasherehekea maadhimisho ya miaka 10 katika sanaa ya muziki.

Magufuli alipiga simu kupitia msemaji wa Chama Cha Mapinduzi Bwana Humphrey na kumsifia kuwa yeye ni mwanaume.

Katika mtandao wa Insta, Diamond amefunguka na kumsifia sana rais huyu.

“Ni adimu sana kumpata rais ambaye anaweza jali wananchi wake, akawajali vijana, tena hususan kujali wanasanaa…rais ambaye licha ya wingi wa majukumu mazito aliyonayo lakini akatenga muda kutazama onyesho lako…. kama haitoshi, katikati ya show akakupigia na simu juu kukupongeza kwa kazi uifanyayo.. lakini pia kuwasalimu na kuwatakia Kheri watu waliohudhuria show hio…” Alisema Diamond.

Image result for diamond magufuli

Jinsi ya kuepuka kutongozwa kwenye maeneo ya burudani

 “Ni Jambo la kipekee na inataka rais mwenye roho ya kipekee sana…Rais ambaye si mjivuni na mwenye upendo wa dhati kwa nchi na wananchi wake….Shukran sana sana Mh Rais… Daima Nitaendelea kujituma na kuipigania sanaa yetu ili izidi kuleta Sifa na heshima Nchini lakini pia kuzalisha ajira zaidi kwa vijana wenzetu…” Alisema Diamond Platnumz.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments