DISARMED AND HOPLESS: Wafahamu Viongozi 7 watakaopokonywa ulinzi wa polisi na Bunduki .

disarmed
disarmed
  Viongozi kadhaa  walio na kesi kortini au sakata zinazowatilia doa na mkondo wa sheria huenda wakapokonywa ulinzi wa polisi kufautia agizo la Inspekta mkuu wa Polisi Hilary Mutyambai . Mutyambai amesema wote walio na kesi za kujibu kortini kwa sababu ya vitendo vya uhalifu au kesi za kujibu watapokonywa walinzi  ambao ni maafisa wa polisi pamoja na leseni zao za kuwa na bunduki . Baadhi ya Viongozi ambao huenda wataathiriwa ni agizo hilo ni

BABU OWINO

Mbunge huyo wa embakasi mashariki  ameshtakiwa leo kwa jaribio la kumuua  DJ  Evolve katika eneo moja la burudani mtaani Kilimani . ameshtakiwa kwa mienendo ya usumbufu  akiwa amejihami kwa bastola .Mbunge huyo alilala seli mwishoni mwa wiki na ataendelea kuwa katika rumande hadi jumatatu wiki ijayo wakati kortoi itakapotoa uamuzi kuhusu kumwachilia kwa dhamana .

 MIKE SONKO

Gavana huyo wa Nairobi  anashtumiw akwa kumpiga teke mkuu wa polisi wa eneo la pwani Rashid Yakub wakati alipokuwa akikamatwa mwezi disemba mwaka jana . stakabadhi ya kumshtaki koritini ina mashtaka matatu dhidi ya gavana huyo .

OKOTH OBADO

Gavana huyu wa Migori anakabiliwa na msaibu si haba kuanzia wakati wa hatamu yake ya kwanza afisini alipokabiliwa na msururu wa kesi za  ufisadi . mwaka wa 2015 tume ya EACC ilitoa ripoti ya kuwafedheha maafisa wakuu ambao wamehusishwa na ulaji rushwa na jina la Obado lilionekana katika ripoti hiyo. Hata hivyo kilichomsukuma ukutani zaidi ni kesi ya mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno .Gavana huyo amekanusha kuhusika na mauaji ya Sharon .

MOSES KURIA

Mbunge huyu wa Gatundu Kusini ameshtumiwa kwa kumshambulia mwanamke mmoja katika afisi za Royal Media Services . Mwanamke huyo amemshtumu Kuria kwa kumshambulia  baada ya kumuuliza kuhusu matamshi aliyoyatoa katika hafla moja huko Kiambu kuhusu chupi za wanawake. Kuria pia ameshtumiwa kwa kutoa matamshi yanayohatarisha usalama wa baadhi ya wakenya .Aliyatoa matamshi hayo kwa lugha ya kikuyu na tayari  walinzi wake wameondolewa .

FERDINAND WAITITU

Gavana huyu wa Kiambu qambaye tayai amefurushwa afisini na waakilishi wa kaunti anakabiliwa na kesi ya  utoaji wa kandarasi kwa njia isiofaa na kusababisha kupotea kwa shilingi milioni 580. Amezuiwa na mahakama dhidi ya kwneda afisini mwake  hadi kesi hiyo  iamuliwe.

AISHA JUMWA

Mbunge huyu wa malindi   yupo mashakani baada ya mtu mmoja kuuawa kwa kupigwa risasi oktoba mwaka jana katika mkutano wa wa ODM ambao aliuvamia  pamoja na wafuasi wake . kisa hicho kilitokea katika boma la mgombea wa ODM wa wadi ya Ganda Reuben Katana   ambaye baadaye alichaguliwa kuwa mwakilishi wadi wa sehemu hiyo . Haijabainika ni nan aliyeftarua risasi  na kusababisha maafa hayo .Jumwa pia anakabiliwa na kesi ya wizi wa shilingi milioni 57 za CDF katika eneo bunge lake .

MOSES LENOLKULAL

Gavana huyu wa samburu  anakabiliwa na mashtaka manne ya wizi wa fedh za umma ,utumiaji mbaya wa maamlaka ya afisi yake ,  na  mkinzano wa maslahi  uliopelekea kupotea kwa shilingi milioni 84.6. Anashtumiw akwa kuitumia kampuni yake yake -Oryx service station -  kutoa mafuta ya petroli na diesel kwa serikali ya kaunti .Hata hivyo ameyakanusha mashtaka yote dhidi yake .