EACC yamchunguza Oparanya

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi inamchunguza gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kuhusiana na madai ya kununua hoteli moja mjini Kisumu kwa kima cha shilingi milioni 250.

Hata hivyo Oparanya ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la Magavana, siku ya Jumapili alitaja uchunguzi huo kama kupoteza muda na kushikilia kwamba hamiliki hoteli hiyo na kwamba hana hata nia ya kuinunua.

“Si miliki hoteli hiyo na sijawahi kuimiliki. Wakitaka kuchunguza,wacha wafanye hivyo,” Oparanya aliambia The Star kwa simu.

Aliendelea kusema: “Hakuna kosa mimi kumiliki hoteli. Hata kama ningemiliki, ningefurahia kusema. Nini mbaya na kumiliki hoteli?”

Oparanya amepongezwa sana kwa kuimarisha maendeleo katika kaunti ya Kakamega na huenda uchunguzi wa EACC rekodi yake nzuri.