Edgar Obare afikishwa katika mahakama ya Kiambu

Obare
Obare
Mwanablogu tatanishi nchini Edgar Obare Jumatatu amefikishwa katika mahakama za Kiambu baada ya kutiwa mbaroni wiki jana .

Obare anakabiliana na makosa ya kuweka wazi data za kibinafsi za  mwanamke Natalie Wanjiru anayefahamika kama Natalie Tewa.

Akiwa mbele ya mahakama hiyo,Obare amekana mashtaka dhidi yake huku akisubiri kubaini hatima yake wakati ambapo mahakama hiyo itakaporejelea vikao vyake saa 2 mchana hii leo.

Obare alitiwa mbaroni Ijumaa akiwa Kisumu na maafisa kutoka DCI ili kujibu madai dhidi yake.

Yanajiri haya baada ya kushutumiwa kwa kuandika ujumbe kwenye  mtandao wake wa Instagram kuwa mwanamke huyo alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanasafiri Dubai kumtembelea kiongozi wa ODM Raila odinga ambaye alikuwa amelazwa hospitalini.

Miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo alikuiwa mbunge Junet Muhammed na gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.

Obare alilazimika kukesha katika kituo cha polisi cha Gigiri Wikendi kabla ya kufikisha mahakamani hii leo.