Eliud Kipchoge atuzwa kama mwanariadha bora wa kiume duniani

kipchoge
kipchoge
Eliud Kipchoge na Dalilah Muhammad wametajwa kuwa wanariadha bora zaidi duniani wa kiume na kike mtawalia.

Kipchoge alishinda London Marathon kwa mara ya nne mwezi Aprili kabla ya kuwa mtu wa kwanza kukimbia marathon kwa chini ya masaa mawili mwezi Oktoba.

Muhammad naye alishinda mbio za mita 400 za ubingwa wa dunia kuruka viunzi huko Doha akiwa amevunja rekodi ya dunia mara mbili mwaka huu.

Kipchoge alisema kuwa ana furaha kupewa tuzo hilo kwa mara ya pili sasa.

Alisema,

Mabingwa wa ligi ya Primia Manchester City walirudi msururu wa ushindi baada ya kutoka nyuma na kuwanyuka Chelsea katika mechi ya kusisimua. Wageni Chelsea ambao wameshinda mechi saba ugenini walipata bao la kwanza kupitia kwa N'Golo Kante. Wenyeji hata hivyo walijitahidi na kusawazisha kupitia kwa Kevin de Bruyne kabla ya Riyad Mahrez kuwaweka kidedea.

Unai Emery anaelewa ni kwanini mashabiki wa Arsenal walizomea kikosi chake baada ya kutoka sare ya 2-2 na Southampton shinikizo linapozidi kwa meneja huyo wa Gunners. Kocha mkuu Emery yuko kwenye shinikizo kubwa baada ya msururu wa matokeo mabaya ya ushindi katika mechi mbili tu kai ya 11 za ligi ya Primia walizocheza. Emery anaungwa mkono na usimamizi wa Arsenal lakini ameonywa ni lazima matokeo yaimarike.

Manchester United, Arsenal na vilabu vingine vikuu vya ulaya huenda vikapigwa na butwaa kwa sababu RB Leipzig itakuwa na nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Red Bull Salzburg wa miaka 19 Erling Braut Haaland kwa pauni milioni 25.7 pekee. Kwingineko Crystal Palace inataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud mwenye umri wa miaka 33, lakini huenda masharti ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ikawa kikwazo ya wao kuafikiana.

Manchester United hii leo watapambana na Sheffiled United katika ligi ya Uingereza. Huenda Sheffield United wakalazimka kubadili ulinzi wao kwa mara ya kwanza msimu huu kwani jeraha la kichwa la John Egan linachunguzwa. Kipa wa mkopo Dean Henderson huenda akacheza, kumaanisha kuwa Simon Moore atacheza kwa mara ya kwanza katika ligi hio. Kiungo wa kati wa Manchester United  Scott McTominay hatacheza kwa wiki kadha kutokana na jeraha la mguu, huku Paul Pogba pia akisalia nje. Luke Shaw na Nemanja Matic wameregeleaq mazoezi lakini hawatacheza.