‘Enda ukapikiwe na huyo dem wako!’ Diana amfokea Bahati

9Ymk9kpTURBXy85OWZjMWQ2ZDk5NGEwYTJlMDg0ODU4YzE1YTM5YjdjMi5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE
9Ymk9kpTURBXy85OWZjMWQ2ZDk5NGEwYTJlMDg0ODU4YzE1YTM5YjdjMi5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE
Baada ya Emmah kufichua kitendo cha kuchepuka na kutoka kimapenzi na wanawake nje ya ndoa, staa Bahati sasa ameonyesha hasira na kumfuta kazi. Katika kipindi kinachoangazia maisha halisi ya staa huyu wa muziki, Emmah alimpigia simu mkewe Bahati akilia kwa uchungu.

Soma hapa:

"Imagine nimepigwa kalamu kwa sababu ya kukufichulia siri ya mmeo ya kuchepuka. Alikuja ofisini na kunifuta kazi. Sasa sijui nitafanya nini." alisema kijakazi Emmah.

Katika video hiyo, Diana ambaye kwa sasa ana ujauzito wake Bahati anatoka kwa hasira na kufika katika chumba cha kulala na kuivuta blanketi Bahati aliyojifunika.

"Mbona unalala wakati huu. Mbona umefuta kazi Emmah? Diana alimfokea Bahati.

Kwa upande mwingine Bahati anakasirika kwa kubumburushwa usingizini na kumjibu.

"You want to tell me you just woke me up to ask me why i fired Emmah."

Majibizano kati ya wawili hawa yanazidi na Diana ampasha mmewe.

Soma hapa:

"From today i've employed her as my PA. Unakuwanga na madharau sana. Enda ukapikiwe na huyo dem wako" alifoka Diana.