Esther Arunga akabidhiwa kifungo cha miezi 10 nyumbani katika mauaji ya mwanawe

Aliyekuwa mtangazai Esther Arunga amehukumiwa kifungo miezi 10 nyumbani kuhusiana na mauaji ya mwanawe Sinclair Timberlake.

Jumatatu wiki hii, Arunga alikiri kuwapa taarifa ya uongo maafisa wa polisi ili kumsaidia bwanake Quincy Timberlake kukwepa mashtaka ya mauaji.

Sinclare Timberlate aliyekuwa na umri wa miaka mitatu alifariki kutokana na majeraha ya kupigwa na kifaa butu tumboni.

Mwanawe alifariki akiwa nyumbani kwao Kallangur, kaskazini mwa mji wa Brisbane nchini Australia mwezi Juni mwaka 2014.

Taarifa zaidi:

Babake ambaye wakati mmoja alikuwa mgombeaji wa urais nchini Kenya Quincy Timberlake anakabiliwa na mashtaka ya mauaji.