Ethiopia wapanga mikakati ya kupiga marufuku ukahaba

kahaba
kahaba

Maafisa katika mji mkuu wa Ethiopia Adis Ababa wanaandaa mkakati kupiga marufuku ukahaba na kuombaomba wa mitaani , ikiwa ni hatua ya hivi karibuni katika msururu wa hatua za kusafisha sura ya taifa , imesema ofisi ya meya wa mji huo.

Muswada unaoonyesha sheria za marufuku hizo bado unakamilishwa.

Hata hivyo afisa wa habari wa Meya wa Mji wa Adis Ababa Feven Teshome, ameliambia shirika la habari la AFP amesema marufuku hizo ni muhimu ili kupambana na "matatizo ya kijamii " katika mji huo wenye zaidi ya watu milioni moja.

" Tunakadiria kuwa kuna ombaomba 50,000 na zaidi ya makahaba 10,000 mjini Addis Ababa. Muswada wa sheria unalenga kumaliza matatizo haya ya kijamii ambayo pia yanaleta picha mbaya kwa Ethiopia," anasema Feven.

Kazi ya ukahaba kwa sasa si uhalifu nchini Ethiopia, na Feven anasema pendekezo la kuipiga marufuku mjini Addis Ababa itawahusu tu ombaomba wanaozurura mitaani.

Hii ikimaanisha kuwa haiwezi kutekelezwa katika sehemu kama vile baa , maineo ya kusinga, nyumba za malazi na maeneo mengine ambapo shughuli za ukahaba huwa ni nyingi.

Wafanyabiashara ya ukahaba na wateja wao kwa pamoja watakabiliwa na adhabu ambayo inaweza kuwa ni kulipa faini au kufungwa jela kwa muda fulani anasema Feven.

Mnamo Mei, maafisa wa Ethiopia walitangaza sheria kuhusu matangazo ya biashara ya pombe kote nchini ambapo walipiga marufuku matangazo ya biashara ya pombe na sigara katika maeneo ya umma.

Sheria hiyo pia ilipiga marufuku mauazo ya pombe kwa mtu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 21.

-BBC