Eugene Wamalwa ataka Mudavadi na Wetangula wasaidia ne kuunganisha Waluyha

Waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa amemtaka kinara wa chama cha FordKenya Moses Wetangula na mwenzake wa ANC Musalia Mudavadi kuvunja vyama vyao na kuunda chama kimoja iwapo wangependa kuunganisha jamii ya Luhya.

Akizungumza katika hafla ya kuchangisha pesa kwa wahudumu wa bodaboda mjini Webuye, Wamalwa amesema kuwa itakuwa vigumu kwa jamii ya Luhya kuungana na kuiongoza taifa hili iwapo viongozi wa eneo hilo watazidi kuwa katika vyama

tofauti.

Na kwa habari zingine;

Seneta wa Bungoma Moses Wetangula amemtaka rais Uhuru Kenyatta kuleta fedha za kuwalipa wakulima wa miwa bali si kuwapa wasimazi wa viwanda vya Nzoia na Mumias fedha ambazo wanafuja bila kudai masilai ya wakulima.

Wetangula ametaka usimamizi wa viwanda hivyo kubadilishwa akidai kwamba usimamizi mbaya ndio chanzo cha masaibu ya viwanda hivyo

Wetangula amesema kwamba kamati ya seneti inashughulikia jinsi wakulima wa maindi wameporwa mamilioni ya fedha kwa kuhakikisha walio pora fedha wanakabiliwa ipasavyo na sheria.

Brian O Ojama