Fahamu vyakula unapaswa kula ukiwa na ugonjwa wa saratani

Kabla ya kutibiwa chakula ni muhimu katika mwili wako si chakula tu  bali uwe na utaribu maalum wa chakula haswa kama wewe ni muathiriwa wa ugonjwa wa saratani ambao umechukuwa uhai wa wengi.

Kuna aina nyingi za saratani karika mwili wa mwanadamu.

Saratani imewauwa watu maarufu,watoto,marafiki,wasanii wazazi wa wengi na kuwaacha yatima, endapo umepatikana na saratani usijichukie bali fuata maagizo ya daktari na kula vyakula kama vifuatavyo;

Matunda

Kama mgonjwa wa saratani unapaswa kula matunda baada ya masaa mawili,ili kurudisha damu mwilini na upate nguvu ya mwili.

Matunda hayo ni kama, tofaa, nanasi, maembe,Avacado ili ziongeze vitamini mwilini.

Mboga

Karoti inaongeza vitamini K na Vitamini A, unapaswa kula karoti ikiwa kwa chakula, kama mgonjwa wa saratani karoti ni nzuri katika afya yako, si karoti tu pekee bali, kuna vile malenge,mbaazi na hata nyanya.

Protini

Katika kitengo cha protini kuna vyakula vya aina nyingi ambavyo unapaswa kula ili kuongeza protini mwilini, vyakula hivyo ni kama, nyama,maharage ambayo yamekaushwa,mayai samaki na vinginevyo

Wanga(Carbohydrates)

kuna vyakula kama vile wali,chapati,maharagwe, spaghetti,mkate ,

Ni vyakula ambavyo vinapaswa kupewa kipa umbele ili mgonjwa awe na afya kila wakati

Vinasaidia kwa kupa mwili wako nguvu, na haudhoofiki kamwe.

Si vyakula vyote ambavyo wagonjwa wa saratani wanapaswa kula kwa sababu vingi vinaharibu afya yao