Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Nyali Simon Thirikwa amesema pesa hizo zina noti za kale na mpya .Hamida anaripotiwa kuongoza kundi la watu wanaochapisha pesa bandia linalohudumu Mombasa na Nairobi . Polisi sasa wanamsaka mumewe aliyetoroka wakati wa oparesheni hiyo na ambaye husimamiakanisa moja katika eneo la Tudor na hujifanya kuwa raIa wa Congo . Raia mmoja wa Nigeria aliyekwepa mtego huo pamoja na raia huyo wa Cameroon pia anasakwa. Ripoti za ujasusi zasema Hamida ambaye amepata ushawishi mkubwa kutokana na oparesheni zake ametumia kiasi kikubwa cha pesa alizo nazo kuwalinda wanachama wa genge lake dhidi ya kukamatwa .
Polisi pia wamemhusisha na ulaghai mkubwa wa kuwapunja watu fedha kwa kuwapa tiketi,visa na vibaki feki vya kufanyia kazi na kuwahadaa kwamba wanawatafutia kazi katika mataifa ya mashariki ya kati . Januari mwaka huu polisi walivunja genge la uchapishaji wa pesa bandia lenye uhusiano na wahalifu nchini marekani na kunasa shilingi milioi 6.67 za noti za shilingi 1000 ambazo zilikuwa katika hatua za mwisho mwisho za kutengezwa katika nyumba moja huko Mtwapa .