Familia ya Lumakanda yalilia haki baada ya mwanao kuuawa na mgombezi wa MCA kwa tuhma za kuibiwa kuku

chicken-011
chicken-011
Familia moja kutoka eneo la Headquater wadi ya Lumakanda eneo bunge la Lugari kaunti ya Kakamega inalilia haki baada ya jamaa wao kuuawa na

watu waliokuwa wametumwa na mgombezi wa kiti cha MCA  kwa tuhuma za kumuibia kuku.

Familia hio pamoja na wakaazi wa eneo hilo wamedai kua na ushahidi wa kutosha kwamba Kelvin Mutua mwenye umri wa miaka 24 ambaye alikua

muhudumu wa bodadoda aliuawa na watu waliokua wametumwa na mwanaisiasa huyo.

Kwa sasa familia hio imesema kwamba licha ya wao kutoa lalama kwa maafisa wa polisi na kua na ushahidi wa kutosha kwamba mwanaisiasa

huyo wa chama cha Jubilee kwa majina Neal Sumba alihusika na kifo hicho hakuna lolote limefanyika dhidi yake.