Familia ya watu sita waliofariki katika ajali ya barabara, yazika wapendwa wao

WhatsApp Image 2019-11-12 at 14.54.43
WhatsApp Image 2019-11-12 at 14.54.43
Familia moja kutoka kijiji cha Piave kaunti ndogo ya Njoro imeanza kuwazika wapendwa wao watatu walioangamia katika ajali ya barabara.

Watatu hao ni kati ya watu sita waliofariki katika ajali ya barabara ya Nakuru-Naivasha katika eneo la Marewa walipokuwa wakieleka katika mazishi ya jamaa wao Novemba 4.

Moja wa jamaa wa familia hiyo alizikwa Jumatatu huku wawili wakitarajiwa kuzikwa Jumanne na Jumatano.

Akiungana na wakaazi wa eneo hilo, Kamau Kuria ambaye ni mkurugenzi wa bodi wa usimamizi wa mji wa Nakuru na mwanachama  wa bodi ya GDC  alisema kwamba kijiji hicho kinapitia wakati mgumu kufuatia maafa ya watu wanane kwa kipindi cha juma moja.

"Tumekuwa na wakati mgumu sana kwa kupoteza watu wanane katika kijiji hiki kwa kipindi cha wiki moja. Nilimwambia Gavana wito wenu na akaelewa ndiyo maana alitoa usaidizi wake haraka," Kuria alisema.

Aidha aliwashukuru wakaazi kwa usaidizi wao pamoja na ushauri nasha  kwa familia iliyofiwa.

Kuria ambaye pia aligombea kiti cha ubunge katika eneo la Njoro na kuibuka wa pili, aliwasihi viongozi kuwapa misaada wananchi wanapolemewa.

Akiwakosoa wale wanaojitokeza uchaguzi unapokaribia, Kuria alisema kwamba janga linapotokea familia watu wote pamoja na viongozi wanafaa kujitokeza.

"Tusiwe viongozi wa kujitokeza wakati tunahitaji kura zao. Tusimame pamoja kila mara, kwa kila hali,' alisema.

Miongoni mwa waliokuwepo ni mwakilishi wa wadi Zachariah Kahiro miongoni mwa wengine.