Feki! Feki! Tazama jinsi coronavirus ilivyolipua maisha feki ya ‘kifahari‘ ya baadhi ya macelebs

Celebs
Celebs
Umegundua jinsi mitandao ya kijamii ilivyotulia tangu kuanza kwa janga la corona nchini? Macelebs wengi awali walikuwa wakifurika kila kumbi za mitandao  hiyo kwa picha zilizoonyesha maisha yao mazuri na ya ‘kifahari’ lakini sasa, ni kubaya.

Kitu cha kugundua ni kwamba, watu walioonekana kuishi vizuri sasa hawapo tena na hata huoni picha yao hata moja katika instagram, kwa mara ya kwanza sasa wanaishi maisha ya uhalisia.

 Macelebs wengi na  magwiji  wa matumizi ya mitandao walikuwa wakisafiri kwa discount au ni mabalozi wa brandi tofautitofauti

Hii ndio sababu huzioni picha zao tena wakiwa katika hoteli nzuri  nzuri au nchi za kigeni. Channel zao za youtube sasa zinashika kutu .

Baadhi huzilipia safari hizo  lakini wengi huwa hawalipi chochote  na wale ambao hawatoi hata shilingi moja ndio hujaza mitandao kwa pich za walikokwenda .

Wengi hata wanayajua majumba ya kifahari kwa picha tu na kamwe hawatakubali kwamba wanaishi katika bedsitter  au  nyumba za chumba kimoja .

Picha zao wakiwa katika nyumba za kifahari ati apartments huchukuliwa katika nyumba za rafiki zao  au za kukodi kwa hafla za picha hizo. Hawataki  uone vitu kwa ground ni different.

 Vyakula vya mikahawa

Offcourse kumekuwa na mashindano ya kila mtu kupiga picha katika hoteli nzuri akiwa na chakula mezani au hata akiamka asubuhi akiwa kwenye bathtub au hata kando ya swimming pool .

My friend sasa hivi watu wamekwama  na chakula kizuri ni mtumbo managu na ugali kauka. Msiogope kuweka picha za githeri na hata mutura mkiwa raundi mwenda pale estate .

Filters  za picha ziliwaokolea sana

Kuwa celeb ni jambo zito kwa baadhi ya watu na kuna hadhi ambayo kila mmoja anataka kudumisha. Hakuna anayetaka tuone pimples na acne za usoni. Hakuna anayetaka uone  alama zozote katika ngozi yake na hapo ndipo filter zitafanya kazi .

Hali imekuwa ngumu na wengi sasa wameanza kuweka tu posts za kutupa matumaini maishani. Verses za bible sasa ndio mtindo. Wengi wameshindwa kwenda saluni na  sura  zimebadilika wengine watakushtua mkikutana ufikiri umeona zombie

Halafu kuna wengine ambao wamekuwa wakiziweka picha za sehemu zao nyuma kutuonyesha vile wamebeba, kumbe wameshindwa kurudi kwa wataalam wao kuwapiga sindano za kuongeza mafuta katika sehemu hizo. Ukweli sasa umeanza kujitokeza .

Utagundua wameanza kuwapa picha za TBT  hata kama sio Alhamisi. Si vibaya lakini ukweli lazima usemwe. Hawana picha zao nzuri walizopiga tangu Corona ianze .

My friends, usiwahi kujipa presha bure kuhusu mwili wako, unakoishi au chakula unachokula. Fanya mambo yako kivyako na ujifurahishe kwa njia yako spesheli. Pika na kuni ukitaka nani, Kenya ni yetu lakini  wacha kusumbua watu kwa kuposti picha ya cooker ya jirani na  Dish washer  ya hoteli ulilala 2010.