Felicien Kabuga afikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza baada ya kutiwa mbaroni

Kabuga (kushoto) baada ya kukamatwa nchini ufaransa/ Picha Hisani
Kabuga (kushoto) baada ya kukamatwa nchini ufaransa/ Picha Hisani
Felicien Kabuga, jamaa anayeshtumiwa kwa kuongoza mauaji ya halaiki ya watu mwaka 1994 katika taifa la Rwanda alifikishwa katika mahakama za Ufaransa siku nne baada ya kutiwa mbaroni baada ya kuwa mafichoni kwa miaka 26.

Katika kikao hicho cha kwanza, janadume hilo liliingizwa kizimbani likiwa limekalia kitimaguru ama Wheelchair na alikuwa amevalia barakoa.

Kabuga ameorodheshwa na jumuiya ya kimataifa UN kama kiongozi aliyeongoza makundi ya kuangamiza watu na kueneza jumbe za vitisho na makosa mengine mengi.

Kabuga aliongoza jamii ya Hutu ambayo iliwauwa wakaazi wa jamii ya Tutsis takriban 800,000 kewa zaidi ya siku 100 , jinamizi ambalo lilitajwa kama kubwa zaidi katika historia ya taifa hilo.

Mahakamna hiyo ilikuwa na majaji watatu ambao sasa wanatafakari iwapo watampeleka hadi mahakama za UN. Kesi hiyo itaskizwa Mei 27.

Mawakili wanaomwakilisha Kabuga wametaka uamuzi kufanyiwa Ufaransa na kukashifu mkuu wa mashtaka wa Rwanda kwa kujaribu kuarakisha kesi hiyo.

“Mr Kabuga is an old man, he’s tired and sick,” lawyer Laurent Bayon told the judges. “The prosecutor wants to be rid of Mr Kabuga.”  Alisema wakili wa kabuga

Mkuu wa mashtaka wa UN  Serge Brammertz, amesema uamuzi unakaribia kuafikiwa na huenda jamaa huyo dhalimu akasafirishwa hadi mahakama za Hague bali si Afrika kutokana na masharti ya kutosafiri yaliyowekwa na mataifa mengi.

“is definitely an option” for a first legal phase to be conducted in The Hague, Brammertz aliliambia shirika la  Reuters.

Mchakato wa kumtafuta Kabuga umechukua zaidi ya karne mbili ambao ulikuwa unaendeshwa baina hya mataifa ya Afrikia na Ughaibuni.

Alikuwa anamiliki kituo cha redio ambacho kilikuwa kinaeneza jumbe za kuichochea jamii ya Tutsi .

Amerika ilikuwa imeweka kima cha dolla milioni 5 kwa atakayempata.

Mawakili wa Kabuga aidha wameshikilia usemi kuwa watamuondoa kwa dhamana.

Miongoni mwa watu waliohudhuria vikao hivyo ni mwanawe mvualana.

.