Felicien Kabuga: Mahakama ya Ufaransa imeamuru mfanyabiashara huyo wa Rwanda ashtakiwe katika mahakama ya UN

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa mbele ya mahakama maalum ya Umoja wa mataifa iliopo Tanzania.

Mwanabiashara huyo wa Rwanda anakabiliwa na mashitaka ya kufadhili na kuchochea mauaji ya kimbari ambapo waendesha mashtaka wanasema alifadhili makundi ya Kihutu ambayo yaliwaua karibu watu 800,000 kutoka kabila la Watutsi mwaka 1994.

Soma pia;

Kabuga, mwenye umri wa miaka 87 alikamatwa viungani mwa mji wa Paris mwezi uliopita baada ya kuwa mafichoni zaidi ya miaka 25.

Amekanusha mashtaka dhidi yake na kuyataja kuwa ya uwongo.

Mwaka 2006, jopo la kimataifa la Rwanda lililokuwa likichunguza mauaji hayo lilisema lina ushahidi kwamba bwana Kabuga alizuru nchini Kenya ama hata kuishi nchini humo, ambapo alikuwa akisimamia maslahi yake ya kibishara.

Soma pia;

Miaka mitatu baadaye, Bwana Stephen Rapp, ambaye alikuwa balozi wa Marekani aliishutumu serikali ya Kenya kwa kukataa kumtoa bwana Kabuga.Kulikuwa na ushahidi kwamba bwana Kabuga alihudhuria hafla zilizoshirikisha watu maarufu, alisema madai ambayo Kenya imekana.

Ni wazi kwamba familia ya bwana Kabuga ilikuwa ikimiliki mali nchini Kenya baada ya mali moja kuzongwa na kesi 2015 wakati mkewe, Josephine Mukazitoni , ambaye alikuwa mmiliki mwenza, alipojaribu kumiliki.