Fimbo ya Moi! Gideon Moi aanza kuweka mikakati ya 2022

Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa ameanza kuweka mikakati mwafaka ya kuinua chama cha Kanu katika eneo la Bonde la Ufa baada ya kutia saini maafikiano na chama cha Jubilee wiki jana.

Matawi ya Kanu Rift Valley ambapo chama hicho kina uungwaji mkubwa wa watu, yameidhinisha makubaliona hayo ambayo yalimfanya seneta wa Pokot Magharibi Samuel Poghisio kupewa kiti cha kiongozi wa wengi katika bunge la seneti baada ya kutimuliwa kwa Kipchuma Murkomen.

“We fully support the coalition between our two parties, Gideon Moi and President Kenyatta, and endorse the decision to have Poghisho take over as Senate Majority Leader,” David Chepsiror, mwenyekiti wa Kanu tawi la Uasin Gishu.

Pia maoni hayo yaliungwa mkonoi na viongozi wengine 15 wakiwemo Paul Kibet wa Keiyo Kusini.

“The new arrangement was long overdue because it will help the President achieve his plans for the country instead of having a situation where all his plans are opposed and undermined by people who have selfish interests especially within the Rift Valley region,”amesema  Kibet .

Gideon kwa sasa anafanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa eneo hilo kutoka kwa chama cha Kanu na vyama vingine ili kuleta maambatano kufikia mwaka wa uchaguzi wa 2022 kutokana na mvutano uliopo baina ya rais Kenyatta na naibuye William Ruto.

Ruto kwa sasa ana uungwaji mkubwa wa watu ukanda huo wa Rift Valley huku viongozi Samson Cherargei na Oscar Sudi wakipinga vikali maafikiano baina ya Jubilee na Kanu.

“Even the Political Parties Tribunal has already declared that the so-called coalition illegal, but all the same Kanu is not a factor in either Rift Valley or national politics,” Cherargei alisema.

Sudi amesema kuwa hawatalegeza kamba kuhusiana na hatua ya kumpigia debe naibu rais na kuongeza kuwa idadi kubwa ya watu wanaomuunga mkono nchini haitapungua kamwe.

“We are not interested in small-time politics with non-entities like Kanu. Our focus as a team led by the DP is how to take this country forward because our youth have no jobs and the economy is collapsing,” Sudi aliongezea .

Kifo cha mzee Moi kilimfanya Gideon kupata uungwaji mkono kutoka kwa viongozi wengine baada ya kupokezwa fimbo maarufu ya Nyayo.

Aidha Gideon yuko na nyumba eneo la Soy, mita chache tu kutoka kwa boma la Ruto Sugoi.

.