Forget it !Waiguru adai Kenyatta hatomuunga mkono Ruto 2022 .

Forget it
Forget it
Gavana wa Kirinyaga  Ann Waiguru  amepasua mbarika kwamba rais Uhuru Kenyatta hatomuunga mkono naibu wake William Ruto kumrithi mwaka wa 2022 .

Waiguru amesema rais Uhuru Kenyatta amewaambia wandani wake kwamba anapanga kupuuza ahadi aliotoa kwa Ruto kwamba atampigia debe achukue hatamu za nchi na serikali mwaka wa 2022 . Waiguru ameongeza kwamba rais ameashiria kwamba huenda akamuunga mkono kiongozi wa ODM Raila Odinga kuwa rais baada ya muda wake kutamatika miaka miwili ijayo .

Amesema wakaazi wa mlima Kenya hawafai kuwa wepesi kumuunga mkono mtu ‘kutoka nje’  asiyekuwa na ajenda na kwamba rais Kenyatta ameleta  Ripoti ya BBI ili kuhakikisha kwamba viongozi kutoka eneo la mlima Kenya wanapata fursa ya kuhudumu katika nyadhifa kuu serikalini . Akizunguma kutumia mafumbo ya lugha ya kikuyu  Waiguru amesema ingawaje Uhuru na Ruto walikuwa ‘wakipendana katika ndoa yao na hata kuzaa watoto ,ndoa hiyo haiwezi kuendelea’ .

Waiguru   alishangaa kuhusu nia ya ‘mwanandoa  ambaye ameendelea kutupa matusi kwa mwenzake’ na hivyo basi hawezi kuvumiliwa . Alikuwa akizungumza katika Maya hotel  mjini Sagana  wakati wa mkutano wa ushauriano kuhusu BBI  na wakaazi wa Kirinyaga .  Wabunge wane wa Kirinyaga na waakilishi wengi wa wadi walikosa kuhudhuria mkutano huo . wabunge hao George Kariuki (Ndia), John (Wambugu Kirinyaga central),Gichimu Githinji (Gichugu)  Kabinga Wachira (Mwea),  mwakilishi wa akina mama Wangui Ngirici  na seneta  Charles Kibiru  hakuwa katika mkutano huo mjini Sagana . walidai kwamba hawakuhusishwa katika mpango wa mkutano huo  na walifahamu tu kuhusu eneo la kuandaliwa alhamisi asubuhi .