"Nilijikuta kitandani katika hospitali nchini Uingereza", Tuju aeleza

Raphael-Tuju-696x418
Raphael-Tuju-696x418
Katibu mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju anashukuru Mola kwa kuwa hai baada ya kuhusika kwenye  ajali mbaya katika barabara kuu ya Nakuru alipokuwa anaenda kuhudhuria mazishi ya hayati rais mstaafu Daniel Moi mwezi uliopita.

Tuju akiwa katika mahojiana na gazeti moja la humu nchini, alielezea baadhi ya majeraha aliyopata baada ya kuhusika katika ajali hiyo.

"Nilipoteza damu nyingi na kuvuja damu ndani, mtu kunusurika ajali kama hii ni mapenzi ya Mola hamna njia ingine yeyote ile

Nimefahamu kuwa Mungu ananipenda." Alizungumza Tuju.

"I AM ON THE MEND. AT LEAST EVERY DAY I HAVE MADE PROGRESS. I WAS IN A WHEELCHAIR, THEN ON TWO CRUTCHES, NOW I AM ABLE TO MANAGE WITH ONE CRUTCH AND THIS HAS PROGRESSIVELY HAPPENED EVERY DAY." Alieleza.

"Sikumbuki jambo lolote baada ya hapo, nilijipata kitandani nchini Uingereza hapo ndipo nilitambua nilipokuwa."

Tuju yuko nyumbani kwake Karen ambapo anaendelea kupokea matibabu na kuelezea changamoto ambazo amezipitia.

"Changamoto kuu kwa sasa ni uchungu mwingi, ni uchungu ambao huwezi takia rafiki au mtu yeyote kupitia, hata huwezi tamani adui wako yule mbaya sana kupitia." Tuju Alisema.
"Unapaswa kumshukuru Mungu kwa maana ukiwa hai, hamna mipango au kitu muhimu ambacho kinazidi maisha yako." Alliongeza.