Francis Atwoli afanya kikao na viongozi wa eneo la Magharibi

Maswali yaliibuka miongoni mwa wananhi baada ya Francis Atwoli kufanya kikao na viongozi wa eneo la magharibi huku mudavadi akiachwa nje na kuto hudhuria kikao hicho.

Karata za kisiasa zinaendelea kuchzwa na viongozi wwengi huku nchi ikikabiliwa na janga la corona na kupungusa shughuli za humu nchini na hata uchumi kuenda chini.

Wengi wamepoteza kazi zao zilizokuwa zinawapa mkate wa kilaa siku na hata wafanyabiashara kufunga biasha zao.

Viongozi wa kisiasa waliochaguliwa kutoka eneo la Magharibi mwa Kenya Ijumaa, Mei 29 walikutana na kutangaza msimamo wao kisiasa.

Kundi hilo lilikutana nyumbani kwa katibu wa muungano wa wafanyikazi humu nchini Cotu Francis Atwoli.

Kulingana na duru ndani ya kikao hicho, ajenda kuu ilikuwa ni nafasi ya eneo la magharibi na viongozi wake katika siasa zinzopangwa na kinara wa ODM Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta.

Aidha licha ya Musalia Mudavadi kuwa kigogo wa kisiasa kutoka eneo la Magharibi, kikao hicho cha Atwoli kiliteua viongozi wapya kuendeleza ajenda za eneo hilo.

"Leo tumekutana na kuwateua Francis Atwoli, gavana Wycliff Oparanya na waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa kuongoza jamii yetu katika mazungumzo kuhusu eneo hilo na serikali."Seneta Malala Alizungumza.

Kundi hilo lilisema liko nyuma ya Rais Kenyatta na mwafaka wake wa handisheki na Raila. Viongozi waliohudhuria kikao hicho ni kutoka vyama vyote na pia waliovuma awali kama mfanybiashara Cyrus Jirongo.

Haikubainika iwapo Mudavadi na seneta wa Bungoma Moses Wetangula walikuwa wamealikwa,Wawili hao ndio wamekuwa vigogo wa eneo la Magharibi huku Atwoli akionekana kama mshauri wa eneo hilo.