Fungua duka! Aliniacha ‘ocha’ pekee yangu nikaamua kufungua miguu

legs apart
legs apart
  Ilikuwa mtindo zamani kwa wanaume kuwaacha mashambani wake zao nao wakienda mijini kufanya kazi lakini visa ni vingi jinsi wanaume wengine walivyojipata wakisaidia kazi ya kuwapa tendo la ndoa wake zao na hata ndoa nyingi zilivunjika .

Ila siku hizi imekuwa vigumu sana  kumuambia mwanamke kwamba aishi mashambani nawe ubaki mjini kwa kazi na kuna uwezekano wengi hawana nidhamu ya kuishi mbali na waume au wake zao. Mume akiwa mjini basi kapata ruhusa ya kutoka nje ya ndoa na kila mwanadada lakini Rita Shivaye anasema katu hangeweza kukaa hivyo bila kupewa ngono wakati mume wake  George alipomlazimisha kurejea mashambani Vihiga naye akisalia Nairobi kwa ajili ya kazi .

‘Kila nilipokuwa nyumbani ,nikirudi majirani waliniambia jinsi mume wangu alivyowaleta chumbani mwetu wanawake tofauti tofauti’ anasema Rita

‘ … Na  nikajua kwa nini alitaka niende mashambani ili apate  fursa ya kuendelea na tabia yake, so nilijua pia mimi nikipata fursa nitampa dawa ile ile –Pia mimi nitawafungulia wanaume miguu yangu’ anasema Rita kwa  hasira

Mwaka wa 2019 Agosti basi majibizano kati yao kuhusu Rita kwenda mshambani yalifika kilele.Rita akajiamulia mwenyewe kwamba atakubali kuishi  mashambani lakini katu hatokuwa mwathiriwa bali pia atajipa ujasiri na kukausha macho ili mumewe naye pia asikie kuhusu mambo ambayo atakuwa akifanya na wanaume huko Vihiga na kweli  alizua sakata  nakuambia! Alipofika  mashambani, Rita  mwanzoni alikuwa mke mzuri  na sifa kweli  zikamfikia mumewe  Narobi. Mama mtu alikuwa akienda shambani na kufanya kazi zote pale hadi mama mkwe akaridhika kabisa . Ila kosa aliofanya mumewe ni kurejelea tabia yake ya kuwaleta wanawake wengine  akiwa pekee huko Nairobi. Hapo ndipo Rita alipoamua kwamba anachoweza kufanya mwanamme naye mwanamke anaweza kukifanya kwa ubora zaidi!

Alipokubali kuja mashambani, mumewe alimuahidi kuja nyumbani angalau kila mwisho mwa  mwezi lakini baada ya kufanya hivyo miezi miwili, George aliingia mitini na kuanza tu kutuma pesa kupitia simu .

   ‘Kama mwanamke , tatizo langu la kwanza lilikuwa kwamba iwapo  haoni haja ya kuja nyumbani basi keshapata wa kumridhisha kule mjini’  anasema  Rita

Mumewe alitoa vijisababu vingi vya mbona hakuwa akija nyumbani na baada ya mwaka mzima, Rita akajua sasa hapo ingemlazimu atumie mbinu nyingine ili kumfanya ajue kwamba kweli naye pia alikuwa na chaguo. Alianza mahusiano ya kimapenzi na watu kadhaa kule kijijini na muda si mfupi stori zake zilisambaa mitaani hadi kwa mumewe aliyekuwa Nairobi . Shemeji zake walihakamishwa naye sana wakimtaka kaka yao kumchukua mkewe kutoka mashambani kwa sababu alikuwa akiwaletea ‘aibu’ kule nyumbani .‘Sikubagua wa kulala naye na hata nilimpa  uroda  mchungaji wa ng’ombe  pale kijijini’ anasema Rita . Baada ya kudaiwa kwenda  na wanaume mbalimbali pale kijijini ,hakuna kilichomkwaza mume wa Rita kama  stori iliyosambaa kwamba mkewe alilala na mchungaji wa mifugo .

‘ Alikwazwa sana kwamba nililala na mchungaji wa ng’ombe lakini mimi nikamkumbusha kuhusu ripoti nilizopata kwamba naye pia alilala na mfanyikazi wa nyumbani wa jirani yetu’. Anafichua  Rita. Baadaye mumewe alimua kumrejesha mjini Rita ili kupeuka aibu nyingi ambazo zilikuwa sasa zimeanza kuvuruga fikra zake na ubabe wake kama mwanamme. Mikutano yote ya watu kutoka kwao hapa Nairobi ilizagaa uvumi wa jinsi  anavyosaidiwa na wana kijiji kumtosheleza mke wake na hangeweza kuvumilia. Rita anasema mbinu yake ilizaa matunda na sasa mume amepata somo .

Uamuzi wa  iwapo  wewe na mkeo mnafaa kuishi mbali na kila mmoja unafaa kufanywa kwa maafikiano ili pasiwe na visa vya mmoja wenu kuchovya vya nje   na kusababisha  matatizo katika ndoa .Je,ni vyema kwa mwanamme kumuacha mkewe mashambani kwa ajili ya kazi?