Furaha kijiji cha Sobea, Joyce Wairimu arejea nyumbani tangu vita vya uchaguzi

Screenshot_from_2019_11_15_15_15_58__1573820199_15971
Screenshot_from_2019_11_15_15_15_58__1573820199_15971
Mwanga wa matumaini umeangaza kijiji cha Sobea kaunti ya Nakuru baada ya binti Joyce Wanjiru kurejea.

Joyce alitoweka miaka chache nyuma wakati nchi hii ilijipata katika vita vya uchaguzi wa 2007/08.

Inaripotiwa kuwa Joyce alikuwa na nyanyake katika uwanja wa maonyesho Nakuru sehemu na ambayo ilitengewa wakimbizi kipindi hicho.

Familia yao ilikuwa imehama kutafuta usalama wao kufuatia rabsha hizo.

Kipindi hicho, Joyce alikuwa na umri wa miaka minne na aliweza kuopolewa na maafisa wa usalama na kuwekwa katika sehemu ya kushughulikia watoto eneo la Kajiado.

Juhudi za mchwa kati ya taasisi hiyo inayoshughulikia watoto na idara ya watoto Nakuru zimesaidia kuwapatanisha.

Kulikuwa na hali ya sintofahamu na kutoelewana baada ya Joyce kukosa kufahamu ndugu wa ukoo.

Nyanyake wa miaka 60 hakuweza kuamini macho yake alipokutana na mjukuu wake.

Wanjiru sasa ana umri wa miaka 16.

"Mjukuu wangu! Ni wewe? Siamini. Nahisi kama naota..." Alishangaa nyanyake Joyce.\

"Nilikuwa naomba na matumaini yalikuwepo kuwa nitawahi kuona tena..." Aliendelea nyanya huyu kwa tabasamu tele.

Wanakijiji walifurika boma lao kufurahia kisa hicho cha kushangaza.