Gavana wapongeza Oparanya kuchukua usimamizi kiwanda cha Mumias

Magavana kutoka kaunti za mkoa wa magharibi wanaunga mkono juhudi za gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kuchukua usimamizi wa kiwanda cha Mumias.

Akiongea kwenye maonyesho ya kilimo ya Kakamega, gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati amesema sekta ya miwa ni muhimu kwa uchumi wa magharibi.

Kwingineko

Seneta wa bungoma Moses Wetangula amewataka wabunge kuona kwamba wanatenga fedha za kutosha katika bajeti kununua mahindi ya wakulima msimu wa kuvuna.

Wetangula amesema ni jambo la kufedhehesha kila wakati wakulima kukosa soko kwa jasho la mazao yao huku madalali wakinufaika.