George Ikua afichua kuwa amepata mpenzi mwingine

George Ikua, mumewe aliyekuwa mwanahabari wa kituo cha NTV, marehemu Janet Kanini Ikua ametangaza kuwa amepata kipenzi cha roho yake tena na yuko tayari kuingia kwenye bahari la mapenzi tena.

Janet aliaga dunia mwaka wa 2017 baada ya kuugua ugonjwa wa saratani ya mapafu.

'Ni ukweli niko kwenye uhusiano na nina uhakika kabisa kuwa nataka kuupeleka hadi hatua nyingine." Alisema Ikua.

Akizungumzia kuhusu marehemu mkewe, Ikua alisema kuwa hata kama ameamua kusonga mbele na maisha yake haimaanishi upendo wake kwa Janet umepungua.

Janet atakuwa nami hadi niage dunia, Janet alikuwa rafiki wangu wa dhati na nilipokuwa naanza kazi yangu tulikuwa tunachumbiana na tulikua pamoja.

Mimi ndiye nilimpeleka kwa mahojiano yake ya kwanza ya kazi ya runinga.

Hayo yakijiri, Ikua alifichua mambo matano ambayo yeye hutilia maanani kwanza kabla ya kumuoa mpenziwe.

  1. Kama wawili hao wanaelewa lugha ya mapenzi baina yao.

2. Ikifikia mambo ya kufanya tendo la ndoa, kama wawili hao wanaelewa lugha ya mwingine kwani ni jambo la maana kwenye ndoa.

3.Kuelewa ndoa tofauti, ndoa ya fedha na ndoa ya kivutio.

4.Uzazi, kwa mfano yeye atakuwa mzazi wa aina gani kwa watoto wake?.

5. kama yuko tayari kuheshimu jinsi marehemu mkewe alikuwa kwake.

Kwa haya na mengi soma .