Ghost Mulee, Raila wahudhuria mazishi ya Joe Kadenge

Mtangazaji Jacob 'Ghost' Mulee ambaye ni alikuwa rafiki wa karibu wa Joe Kadenge ni miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria mazishi ya mwenda zake.

Mazishi ya Kadenge yanafanyika nyumbani kwake katika kaunti ya Vihiga.

Mwenda zake Kadenge ni gwiji wa kadanda nchini, na aliaga dunia yapata wiki mbili zilizopita akiwa na umri wa miaka 84, na alisifiwa na wengi kama mwanasoka ambaye aliiletea Kenya hadhi kuu katika nyanja ya soka.

Mulee aliandamana na rafiki zake wa karibu akiwemo, Mahmoud Abbas ambaye alikuwa kipa maridadi wa timu ya Harambee Stars, na wengineo.

Aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga pia ni miongoni mwa wageni na inatarajiwa wachezaji wa soka wa zamani na wa sasa pia watahudhuria mazishi hayo.

Siku ya Junatano, wanasiasa, marafiki wa karibu na familia yake Joe Kadenge, walikusanyika kwenye Kanisa la Friends International kumpa heshima zake za mwisho shujaa huyo.

Binti yake Esther alisema,

Joe alipenda nambari saba, jeresi yake ilikuwa namba saba, gari yake ilikuwa na nambari saba, namba yake ya nyumba pia ilikuwa ni saba na alifariki tarehe saba ya Julai.

Joe Kadenge alikuwa mwanasoka mahiri sana siku zake na aliichezea timu ya taifa Harambee stars kwa miaka 14 baada ya kuanza kusakata boli  miaka ya sitini.

Baada ya kustaafu kutoka soka, Joe alijitosa katika usimamizi wa kandanda ambapo pia alipaa na kuwa kocha wa timu ya Harambee Stars mwaka wa 2002.

Mwenyezi mungu na aijalie nafsi yake na kuipa ujasiri familia na rafiki zake.