Wamesema hatua hiyo italeta uoja na kuboresha ustawi wa kijamii na kiuchumi katika eneo la na kote nchini
Wanataaluma hao ni pamoja na Daniel Yumbya wa Kenya Medical Practitioners and Dentists Council, ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamba Professionals Forum .
Wengine ni afisa mkuu mtendaji wa Kenya Film Classification Board Erick Mutua, mwenyekiti wa Kenya Medical Training College Philip Kaloki, Aliyekuwa mwenyekiti wa EACC Mumo Matemu na mhadhiri wa chuo kikuu cha Kenyatta Prof Donald Kombo,South Eastern Kenya University VC Prof Geoffrey Muluvi, aliyekuwa mkurugenzi wa KMTC Dr Timothy King'ondu, Mkurugezi wa Ease of Doing Business John Mwendwa na Prof Julius Kyambi wa chuo kikuu cha UoN .
Zaidi ya wanachama 50 wa baraza kuu la chama cha Wiper waliimpa Kalonzo Idhini ya kukubali ushirikiano wa kufanya kazi na c vyama vya Jubilee na Kanu .
Baraza kuu la chama hicho liliongeza kuwa pindi mkataba huo utakapoafiwa ,utatiwa saini na mwenyekiti wa chama Chirau Ali Mwakwere na katibu mkuu Judith Sijeny.
Wanataaluma hao wamesema wanaunga mkono kikamilifu ushirikiano hu kwa sababu maendeleo na siasa yanakwenda sako kwa bako .
Waliongeza kwamba tangu Kenya kujinyakulia uhuru ,eneo la ukambani limekuwa likipata tu maendeleo yafaayo kwa kushirikiana na serikali iliyo madarakani .