Habari 5 zilizowashtua wengi mwaka wa 2019

Mwaka huu wa 2019 umekuwa na mambo mengi, mengine ya kuchosha, kufurahisha, kusherehekea na pia mengine ya kuvunja moyo.

Tunakuangazia habari 5 ambazo ziliwashangaza na kuwashtua wengi;

1.Jamaa kamla mbwa

Jamaa kwa jina Martin Munene kutoka mtaa wa Magundu kaunti ya Tharaka Nithi aliwashangaza wanakijiji baada ya kuchinja na kupika mbwa.

Munene alieleza kuwa alikaa siku tatu bila kula, tukio ambalo lilichangia yeye kufanya kitendo hicho manake njaa ilikuwa imemzidi. Munene alikula mbwa huyo ili angalau apate nguvu ya kuendelea kutafuta kazi ili afadhili mahitaji yake ya kila siku.

2. Kisa cha stowaway 

Kisa kingine cha kushtua ni baada ya kubainikia kuwa Cedric Shivonje Isaac aliyeaminika kuanguka kutoka kwa ndege aina ya KQ Boeing kabla haijatua mjini London mnamo juni 30 mwaka huu, yuko uhai.

Kwa upande mwingine jamaa ambaye mwanzoni alikuwa ametambulika kama Paul Manyasi hakuwahi tambulika.

3. Jamaa akatwa ulimi na mpenziwe

Wapenzi wawili mjini Naivasha walikuwa wakijivinjari kabla ya ugomvi baina yao kuzuka. Hata hivyo walianza kupigana busu baada ya kusuluhisha matatizo yao.

Mwanadada hapo aliamua kuuma na kukata kipande cha ulimi wa mpenziwe na kumeza kabla ya kutorokea eneo la Karagita.

Mmoja wa viongozi wa eneo hilo Solomon Mwangi alisema kuwa hawajui kiini cha mwanamke huyo kutekeleza kitendo hicho.

''After biting off a very big chunk of the tongue, the woman swallowed it and fled leaving the man writhing in pain and he was rushed to the hospital.
The two had been drinking for sometime when the man started kissing the woman and it’s not clear what caused her to turn against her lover.

The man cannot talk as a big part of his tongue is missing while the suspect responsible for the attack has gone missing,” Alisema Mwangi.

4. Akothee kuamua mahala atakapopumzishwa

Akothee alichapisha picha ya jumba lake la kifahari huku akionesha mahala atakapotaka kuzikwa huku akiandika;

‘SEE WHERE I WILL BE BURIED WHEN THAT TIME COMES 😂 I HAVE LIVED THIS LIFE FOR REAL 💪MWANAMKE SINGOL NI KUJIPANGA! UJIPANGE AMA MAISHA IKUPANGE, AMA UPANGIWE CHAGUO NI LAKO ⛔’

5. Sonko kuagizwa apumzike kitandani baada ya kuvamiwa na maafisa wa EACC

Gavana huyo wa Nairobi alitiwa mbaroni Voi.

Baadaye alizuiliwa kwa siku kadhaa kabla ya wakili wake kuandikia mahakama wakisema kuwa ameagizwa na daktari kupumzika baada ya kuvamiwa wakati alipokuwa akikamatwa.

Dakt Esther Nafula Wekesa katika ripoti yake aliandika,

‘MIKE MBUVI SONKO IS A PATIENT CURRENTLY UNDER MY CARE.

HE WAS ADMITTED TO  WITH A DIAGNOSIS OF HYPERTENSIVE URGENCY, SOFT TISSUE INJURY TO THE LEFT CHEST WAL BDATERAI HIP OSTEOARTHNES.

HE HAD NO PREVIOUS HISTORY OF HYPERTENSION. HE WAS STARTED ON ANTIHYPERTENSIVES AND ANALGESICS AND LATER DISCHARGED TO CONTINUE WITH TREATMENT AT HOME.’

Wengine wetu hujipata hadi kazini wakti tunaugua hapa na pale, kwani ye alikua mgonjwa wapi?