Mbunge wa Funyula asema ya kwamba kamati la sukari ilipewa muda mfupi

Mbunge wa Funyula Oundo Mudenyo ambaye pia ni mmoja wa kamati ya bunge la kitaifa la kilimo na biashara amedai kuwa muda ambao kamati hiyo ilipewa kufanya uchunguzi kuhusu sakata ya sukari ya madini ya mercury ulikuwa mfupi.

Mudenyo amesema kuwa walihitaji muda zaidi wa kuwahoji wahusika mbali mbali kabla ya kutoa ripoti kamilifu.

Akizungumza katika shule ya upili ya wasichana ya nangina, mbunge huyo amekanusha madai kuwa kamati hiyo ilipewa hongo huku akisisitiza kuwa hakuna sukari iliyo na madini ya sumu humu nchini.

Leonard Acharry Odhiambo