Mtoto auawa kwa kuiba shs500 Kakamega

Mwanamume wa miaka arobanne mjini Kakamega anasemekana kumpiga na kumuua mwanawe mvulana wa miaka kumi na mitano.
Kijana huyo alikuwa mwanafunzi wa darasa la nane, alipigwa kwa madai ya kuiba shilingi mia tano. Walioshuhudia kisa hicho walielezea kilichotokea.
Jirani mmoja alielezea;
'Mzee akaingia kwa mtoto akaanza kukanyaga bila kujua kuwa ni mtoto wake,
Mwingine akaonyesha akasema;
'Mama anakuwanga mshonaji wa nguo, na anaweza kuwa aliambia mzee kwamba mtoto alichukua pesa, mtoto ni wa kambo, mama ni wa kambo.'
Shahidi mwingine akaelezea akasema;
'Alipiga uyo mtoto, akaambia mama yake, nishikie uyu mtoto niende kuleta gari, akapeleka uko hospitali, akapiga simu akasema mtoto amekufa, amepeleka mortuary, sisi tumeshangaa sana, shilingi mia tano, na uyu ni mtoto wanafunzi amejoin class eight,
Kulingana na wakazi, pesa hizo zilikuwa za mamake wa kambo, jambo lililomghadhabisha babake.